Tazama ilivyo vyema kuwapenda wengine - Ujumbe wa Papa wa mapema Alhamis
Mapema Alhamis hii, Mama kanisa akiadhimisha Siku Kuu ya Jina Takatifu Sana la Maria,
Baba Mtakatifu Francisko aliongoza Ibada ya Misa katika kanisa dogo la Mtakatifu Martha
hapa Vatican, ambamo katika homilia yake alisema, Wala hatuhitaji kuhoji mengi juu
ya uzuri wa Siku Kuu ya leo kwani hakuna asiyeutambua uzuri wa Jina Takatifu Sana
la Maria. Wema wa Mama Bikira Maria, hutufanya sote kuelewa mafundisho mengi ya Yesu,
katika namna tunazopaswa kuyaishi.
Papa aliasa pengine inaweza kuonekana ni
maisha yenye orodha ndefu na ngumu kuiishi, kama ilivyo amri kuu, Mpende adui yako
na mtendee mema , na yule anayekupiga kofi shavu moja mpe na la pili , na yule anataka
kuchukua joho lako mpe na kazu pia. , Ni maneno mazito haya , Papa alisema . Lakini
yote haya kwa namna zake mbalimbali, Bikira Maria Mtakatifu, aliuishi ukweli huo
, Mama aliye neema ya yote na neema ya unyenyekevu, jina linalong'ara kuliko majina
yote, Maria nyota ya asubuhi inayowaangazia na kuwaongoza wafuasi wote wa mwanae kuuishi
upendo wa kweli wa Mungu.
Papa aliendelea kusema, "tunaweza kutafakari na kuelewa
mafundisho ya Yesu , iwapo mioyo yetu, na iwapo nia yetu ni pamoja na Yesu, mshindi,
aliyetushindia mauti, dhambi na dhidi ya utendaji wote wa shetani, na ili nasi
kama waamini wake, tuweze kutenda kama Yesu anavyotutaka. Na hili linahitaji si mengine
kama Mtume Paulo alivyosema: ni kuishi maisha ya upole, unyenyekevu, wema, huruma,na
bila ya kujikuza. Kama hatukazi nyuso zetu katika kumtazama Yesu , basi hatuko pamoja
na Yesu, na hatuwezi kutenda kama anavyotaka. Kuwa na Yesu ni neema, ni neema inayotokana
katika kutafakari sana sura ya Yesu".
Papa alieleza na kushauri kwamba
, inafaa kutenga muda wa ukimya na kufikiri kwa makini juu ya Yesu, na kw akufanya
hivyo tunapata nguvu ya kuwa nae. Yeye mwenye aliye uweza wote, huayatimisha pia yale
yaliyotupungukia. Lakini ili kupata neema hii , tunapasea kuyaweka maisha yetu yote
kwa Mungu kupitia Kristu .Ni kuitafakati sura halisi ya Yesu aliye mwilishwa na kukaa
kwetu katika hali ya ubindamu, akiyaishi maisha yote ya furaha na mateso. ili tuwweze
kufanana nae hatuja njia nyingine, ni kuyapita mapito yake kama ilivyokuwa kw Mtakatifu
Sana Bikira Maria Mama yake alivyoziishi siku za furaha huzuni na kutukuka kwake baada
ya kifo na madhulumu ya binadamu. Vivyo hivyo, kwa mfuasiw a kweli wa Yesu hakuna
njia nyingine ili kuishi na kutembea pamoja katika hali zote.
Ili tuweze kuwa
Wakaristu wazuri, tunapaswa kuutafakari umwilisho wa Yesu tukilinganisha na ubindamu
wa wa watu wateswa, kwa ajlli ya shuhuda kwa watu wote, tukisamehe na kumtafakari
Yesu Mteswa, anayeonekana katiak sura ya jirani anayeteseka. Ni kuyaficha maisha
yetu katika maisha na madonda ya Yesu Kristu , Mungu aliyejishusha, kama anavyotushautri
Mtume Paulo , ni katika kutenda kwa wema, unyenyekevu,upole, ukarimu na saburi.