2013-09-10 09:24:41

Tumaini la Mkristu ni mwili wa Yesu katika Ekaristi.


Baba Mtakatifu Francisko Jumatatu,akiongoza Ibada ya Misa katika kanisa dogo la Mtakatifu Marta mjini Vatican alisema, Fadhila ya matumaini, pengine haifahamiki au kueleweka kwa ufasaha zaidi kuliko ilivyo imani na upendo, na aliasa tumaini lisichanganwe na upendo na huduma.

Kwa Mkristo , matumaini ni Yesu mtu katika Ekaristi na Neno lake . Tumaini ni zawadi kutoka kwa Yesu; matumaini ni Yesu mwenyewe, kama lilivyo jina lake, na ni uweza wa kuokoa na kufanywa upya kila maisha, Papa Francis alisema katika homilia yake . Lakini siyo aina ya tumaini ambalo kwa kawaida kwa akili ya kibinadamu huwa na hisia nusunusu, kwamba ni tu matumaini, kama ilivyo tabia ya binadamu, katika mwelekeo wake wa kutegemea mambo mengi.

Papa alirejea somo la Injili , ambamo Yesu anaponya mtu mwenye mkono aliyepooza na kukosoa walimu wa Sheria na Mafarisayo , Yesu alionyesha hao jinsi ya wao wasivyoijua, njia ya kuwaweka watu huru . Uhuru na matumaini, Papa alisema ,ni kutembea pamoja na Kristu , na mahali ambapo hakuna matumaini , hapana uhuru. Papa alifafanua kwa ishara ya uponywaji uliofanywa na Yesu , inatuonyesha nguvu ya mpya katika njia ya kumweka mtu, kuwa na uhuru kamili.
.
Yesu, matumaini,hufanya upya kila kitu. Yeye daima ni muujiza usiokuwa na mwisho . Kristo, Papa alisema , ni mjumuisho wa miujiza yote ya ufanywaji upya katika Kanisa ,katika maisha yangu na maisha yako na katika maisha yetu wote iwapo tunaamini. Kristo ni kila sababu ya tumaini letu , ni tumaini lisilo shaua.

Amesema , tumaini ni jambo jingine , si jambo la kubumba, bali tumaini ni zawawdi ni zawadi ya Roho Mtakatifu, kama alivyosema Mtakatifu Paolo, kamwe tumaini halipotei. Tumaini kamwe halipotei kwa sababu ni zawadi anayotupatia Roho Mtakatifu. Mtume Paulo anasema tumaini lina jina, nalo ni Yesu. Hatuwezi kusema tuna matumaini katika maisha ya milele au tuna matumaini kwa mungu bila ya kuwa na imani kwa Mungu na Yesu Kristu.

Baba Mtakatifu pia alitoa neno kwa viongozi wa dini wenzake, akisema, inasikitisha kuona Padre hana tumaini. Na hufurahisha kuwaona wale wanaohitimisha safari ya maisha bila ya kuwa ya kuwa na msimamo , lakini wakiwa na tumaini thabiti. Papa aliwataka Mapadre katika maisha yao yote, waonyesha tumaini hili katika Yesu, tumaini lenye kuyabadili maisha yote.

Alieleza na kutaja tumaini kubwa la Mama Maria kwa mwanae ,kuwa mfano wa kuigwa na wafuasi wote wa Kristu. Hata nyakati za giza nene la maisha, alisema, Maria alibaki na tumaini hilo. Tumaini lenye uwezo wa kubadili yote kuwa mazuri.








All the contents on this site are copyrighted ©.