Vita ya Syria, vinakuzwa na soko la biashara haramu ya Silaha
Vita ya Syria ni vita vya biashara haramu ya silaha, isiyojua ubinadamu. Baba
Mtakatifu Francisco, Jumapili wakati wa sala ya Malaika wa Bwana, aliendelea kutoa
wito wa amani kwa dunia , kupitia mafuriko ya watu waliokuwa wamekusanyika katika
uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro Vatican. Alisema na tuendelee kusali na kutenda
kwa ajili ya kufanikisha amani , na hasa kusitisha ukatili wote wa kivita unaofanyika
Syria. Papa alirudia kutoa ombi lake akiwa bado amemezwa na mvuto wa mafungo
na mkesha wa sala wa Jumamosi , aliyo ongoza kwa ajili ya kuombea amani Syria, Mashariki
ya kati na duniani kote. Ilikuwa hasa kuhamasisha usitishaji wa vita vya wenyewe
kwa wenyewe katika taifa la Syria, ambavyo kwa sasa vimeingizwa katika mtengo wa
biashara haramu ya silaha.
Papa Francisko aliendelea kutafakari picha ya
amani duniani, akisema kwa hakika amani imetiwa uvuli na nia binafsi, zenye wivu
na chuki, ubinafsi unaorarua moyo wa udugu na urafiki. Matokeo yake ni utendaji
mbovu dhidi ya maisha ya watu na ubinadamu , kama ilivyo sasa Syria na Mashariki ya
kati. Mgogoro wa kisiasa umeingia katika mtengo wa mfumowa mashindano ya biashara
haramu ya silaha.
Hii ni hatari kubwa na watu wote ni lazima wasema hapana.
Hapana kwa choyo, wivu, chuki, majivuno na na vinyongo na utengano , kwa kuwa havisaidii
kitu, bali ni uvurugaji tu, wa amani na utulivuna ustawi wa jamii. Ni kujinasua
katika mtego huu wa biashara haramu ya silaha.
Papa kwa nguvu zote alipaza
sauti yake akisema, Sasa chuki basi kati ya watu . Sasa basi,
kwa vita inayopiganywa kumbe ndani mwake , mmefichika nia na malengo binafsi, yasiyokuwa
na manufaa kwa jamii . Huu wa wakati wakuskiliza kilio cha watu wenye
mapenzi mema, waliozama katika mafungo na sala, kuombea amani Syria.
Papa
alihoji, katika mtazamo wa kina, vita inasaidia nini ? Kama tu siyo kuleta ghasia
na kuivuruga jamii ? hakuna vita yenye kuletea mema jamii na hasa katika ulimwengu
wa sasa, ambamo wengi wanasubiri kwa hamu nafasi ya kuuza silaha zao walizozalisha
kwa wingi lakini hawana tena soko la kuuza silaha hizo. Hivyo ni lazima jamii iwe
macho kwamba, machafuko kidogo ya jamii kudai haki , inakuwa ni nafasi
kwa wafanyabashara ya silaha kujipenyeza na kukuza machafuko hayo, ili waweze kuuza
silaha zao. Baba Mtakatifu aliendelea kuasa kwamba, kuna mambo mengi mabaya
yanayoletwa na biashara haramu ya silaha. Na daima utendaji wa biashara haramu ya
silaha, huzua vita kwa ajili ya kupatikana kwa soko la kuuza silaha. Alieleza soko
hili, sababu halisi ya jumuiya ya kimataifa, kupigana nayo, tena kwa mshikamano na
umoja thabiti, bila ya kutafuta faida binafsi , bali kwa ajili ya amani na mema kwa
watu wote.
Kwa maelezo hayo, Baba Mtakatifu alimalizia hotuba yake na wito
wa kusitishwa mara moja ghasia zinazo mwangamiza binadamu, na mali Syria, na Misri.
Na tusali ili kwamba Misiri Wakristu na Waislamu , wajiingize kawtiak utendaji wa
kujemba amani na mapatano ya kitaifa kwa ajili ya manufaa yao wote. Ni wazi njia ya
kufikia manai kamaili na mapatano ni defu yeny kuhitaji uvumilivu, hekima na busara
. Pia ameitaka jumuiya ya kimataifa kufanya kazi na majitolea mapya kwa ajili ya ufumbuzi
wa mgogoro wa mgawanyiko ulio rarua raia wa Syria, na kwingineko duniani.
"Natuendelee
kusali bila ukomo, kuomba amani na utulivu duniani.
Baba Mtaktifu mwanzoni
mwa hotuba yake, alirejea tukio la kutangazwa kuwa Mwenye Heri , Mtumishi wa Mungu
Maria Bolognesi, ambaye aliyatolea maisha yake yote katika kuhudumia wengine na hasa
masikini na wagonjwa . Aliyeweza kushiriki ktiak mateso ya wengine katika kina cha
mateso ya Yesu Mfufuka.
Papa alitolea shukurani zake za kwa Mungu kwa ajili
ya shahidi huyu wa Injili, Mwenye Heri Maria Bolognesi. .