2013-09-09 15:19:07

Ujumbe wa Papa kwa wamiliki na wafanyakazi katika Sekta ya Madini duniani


Baba Mtakatifu Francisko , Jumamosi iliyopita, alipeleka salaam zake za matashi mema kwa wamiliki wa Makampuni , viwanda na migondi na wafanyakazi katika sekta ya madini. Salaam za Papa , zilitiwa sahihi na Katibu wa Nchi ya Vatican , Kardinali Tarcisio Bertone na kutumwa kwa Kardinali Peter
Turkson, Rais wa Baraza la Kipapa, kwa ajili ya Haki na Amani.

Baraza la Kipapa kwa ajili ya Haki na Amani, bila ya kujali itikadi na imani za wakuu na wafanyakazi wa Migodoni , huitisha mkutano huo, kwa ajili ya kujadili matatizo ya kimaadili katika shughuli zao, hasa barani Afrika na katika nchi nyingine dunia. Mkutano unawakusanya pamoja pamoja , viongozi wa mashirika mengi ya kimataifa yanayohusika katika sekta hii - Wakristo, wafuasi wa dini nyingine, na wasio waumini – kufanya tafakari juu ya utendaji wao na mchango wao, katika maendeleo na usitawi wa jamii, wakiwa karibu na Halifa wa Petro.

Mkutano huu ilikuwa ni sehemu ya adhimisho la kila mwaka, tarehe 7 Septemba ambayo ni Siku ya Sekta ya Madini duniani, kwa ajili ya kutoa angalisho makini zaidi katika uwanja wa Sekta ya madini duniani, na mada ya mwaka huu imeangalishwa zaidi katika suala muhimu la maadili kwa ajili ya kutunza mazingira na mahusiano ya kijamii katika sekta ya madini. Siku hii iliteuliwa na kuwa siku ya Sekta ya Madini na Baraza la Kipapa kwa ajili ya amani na haki.
Ujumbe wa Papa umetaja umuhimu wa mkutano huo, kwamba si tu, uwezo wake wa kukutanisha viongozi wenye kuwa na imani mbalimbali, lakini pia ikiwa ni tukio ambamo watendaji wakuu wa sekta ya madini , wameweza kukutanika pamoja karibu na Khalifa wa Mtume Petro , kutafakari juu ya mambo muhimu kwa binadamu na mazingira yake. Mkutano uliochunguza kwa kina, umuhimu kimaadili katika yale yanayopaswa kufanywa, ili kwamba sekta hii iweze kutoa mchango mzuri daima katika maendeleo shirikishi ya binadamu .

Papa aliwataka wale wote wanaohusika na Sekta ya madini kuungana nae katika sala . Na aliwapa baraka zake wote wake wa waume, akiwataka watenda kazi yao kwa hekima na busara, wakizingatia udumishaji wa anuai na mazingira mahalia kwenye maeneo yakazi zao na hasa migodini.

Baraza la Kipapa la Haki na amani, liliitenga siku hii 7 Septemba , Kila mwaka, ili dunia iweze kufanya tafakari za kina katika utendaji wa Sekta ya madini. Ni Siku inayolenga kutazama halisi za mazingira ya utendaji wa makampuni ya migodi na jamii mahalia , kwenye utendaji na shughuli za sekta ya madini kilasiku.


Katika mkutano huu, baadhi ya wajumbe walioshiriki Mkutano ni kutoka baadhi ya Makapuni mashuhuri ya migodi ya madini duniani kama African Rainbow Mines, Anglo American , AngloGold Ashanti, Areva , Baker Hughes, BHP Billiton , China Minmetals Corporation, Curis Resources, Fortescue , MMG , Newmont , Rio Tinto na Zamin Resources.

Washiriki wengine ni wawakilishi wa Kanisa wenye ujuzi katika masuala ya madini , akiwepo pia mjumbe kutoka Sekretarieti ya Nchi ya Vatican, pia kutoka Baraza la Kimataifa la Madini na Migodi, , Baraza la Dunia la Migodi ya dhahabu , Shirika la Caritas Internationalis na Oxfam America. Ni Mkutano ulioshrika wajumbe 40 kutoka pande mbalimbali zai dunia.

Ujumbe wa Papa kwa mkutano huo, pia uliotoa shukurani za dhati kwa mikutano ya awali, iliyojumuisha watendaji madini na Baraza la Kipapa , ambamo waliweza kujadili changamoto na masulaa nyeti yanayo husika na sekta hii ya madini .Na hivyo ameomba katika mkutano huu , kwa utambuzi wa makosa ya nyuma, makosa hayo yasirudiwe, mfano utafutaji wa faida binafsi bila kujali hasara zinazofanyika katika mazingira. Au kuwa na mipango ya uwekezaji wa kiuchumi wenye harara za kutafuta manufaa binafsi bila kujali wakazi asilia katika maeneo wanakofanyia kazi. Amewataka, watafakarti changamoto zinazokabili sekta ya madini, na ni yapi yanaweza kuwa malengo ya kweli katika sekta hii, na jinsi gani, wenye kuamua wanaweza kutoa maamuzi yanayofaa jamii kupitia ushirikiano kwa ajili ya ufanikishaji malengo ya muda mfupi na yale ya muda.

Papa amehimiza kwanza kabisa, kuhakikisha mafao bora kwa wafanyakazi wote ikiwemo kuzingatia haki zao, kwa mujibu wa Masharti na kanuni za Shirika la Kimataifa kwa ajili ya Kazi duniani. Na Pia kuhakikisha , kwamba wanajenga moyo wa mshikamano na umoja katika kutafuta faida , ikiwemo kulinda mazingira, kama ivyotakiwa katika ngazi zote za kimkoa na kimataifa na pia kutoa mchango wao, katika kuhakikisa amani na utulivu vinadumu katika maeneo yao ya kazi.


Kardinali Tarcisio Bertone , alitao salam hizo kwa niaba ya Papa , kwa watendaji wote katika sekta ya madini ambao walikusanyika Ukumbi wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Haki na Amani, ili kujadili matatizo ya kimaadili katika shughuli zao, hasa barani Afrika na katika nchi nyingine dunia.

Ni mkutano unaofurahisha kwamba wajumbe wakiwa viongozi wa mashirika mengi ya kimataifa yanayohusika katika sekta hii - Wakristo, wafuasi wa dini nyingine, na wasio waumini – hufanya tafakari pamoja , juu ya utendaji wao na mchango wao katika maendeleao na ustawi wa jamii wakiwa karibu na Halifa wa Petro.








All the contents on this site are copyrighted ©.