2013-09-07 11:07:30

Mashahidi wafia dini Hispania kutajwa Wenyeheri


Watawa 68 ni kati ya watu 522 watakaotangazwa kuwa wenye heri na Mama Kanisa hapo tarehe 13 Oktoba 2013, mjini Tarragona Uhispania. Watu hao 522 ni wafia dini wa Hispania wa karne ya XX. Haya yamebainika kutokana na ujumbe wake Askofu Mkuu wa jimbo la Burgos, Mons. Francisco Gil Hellín utakaosomwa kwenye Maparokia yote jimboni humo hapo siku ya Domenica, tarehe 8 Septemba, 2013.

Kwenye ujumbe huo, Mons. Gil Hellìn amewaalika wakristo wote wa jimbo lake kuhudhuria sherehe hizo za kihistoria nchini humo, akisema kwamba baadhi ya mashahidi hao wa imani walitoka kwenye majimbo ya Levante, bastantes na Madrid; na Kataluña, Aragón.

Naye Baba Mtakatifu Francisko atawakilishwa kwenye sherehe hizo na Kardinali Angelo Amato, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la kuwatangaza waamini kuwa wenyeheri na watakatifu ambazo.

Mons. Hellìi amesema kwamba Mama Kanisa daima amesadiki kwamba wafia dini, ni watu waliomwaga damu yao kwa ajili ya imani, ambayo ndio ushahidi wa juu zaidi wa mapendo, wanaunganisha kabisa Kristo na watu wake. Kwa sababu hiyo wanaheshimika na kukumbukwa kwa namna ya kipekee sana (katiba ya Sheria za Kanisa, na. 50).

Ni jambo la kutia moyo hasa kwenye mwaka huu wa imani uliotangazwa na Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto wa XVI na ambaye anaandika kwenye barua yake ya Kichungaji ya Mlango wa Imani (Porta fidei, n. 13) kwamba “mwaka huu ni wakati muafaka wa kuirejea historia ya imani, ambayo imejaa mafumbo kwani ndaniyake mmechanganyika utakatifu na dhambi”.

Kwa kuwakumbuka wafia dini hasa ndani ya mwaka wa imani ni ishara kwamba Kanisa linatambua utakatifu wa wana wapenzi wa Mungu waliojitoa kidete kwa mapendo na linawapa wote walio safarini moyo wa matumaini wakitambua kwamba huruma ya Mungu imeishinda dhambi. Mwaka wa imani ni mwaka pia wa neema na baraka kwa Kanisa na jamii nzima, na hivyo ni mwaliko kwa watu wote kuwatazama wafia dini ambao ni mifano ya imani, ya mapendo na hata ya huruma ya Mungu kwa wanadamu.











All the contents on this site are copyrighted ©.