2013-09-05 14:47:22

Mipango ya ujenzi wa Kanisa la Kianglikan Gahini, yakamilka


Ujenzi wa Kanisa la Kianglikan la Gahini wilayani Kayonza Rwanda, utatumia kiasi cha Fedha ya Rwanda billioni moja hadi kukamilika. Denisi Karera , Mkuu wa Kamati kuu ya Kanisa , ambaye pia ni mkuu wa tume kwa ajili ya kazi ya ujenzi wa kanisa hilo, ameleeza hivi karibuni kwamba , maandalizi ya ujenzi wa kanisa hilo karibu yamekamilika na kazi zinatazamiwa kuanza tangu mapema Desemba mwaka huu. Ujenzi huo utachukua takriban mwaka mmoja kukamilika.

Kwa wakati huu waamini katika eneo hilo wanatumia kanisa dogo lililojengwa miaka 50 iliyopita na hivyo sasa halikidhi mahitaji ya Ibada katika eneo hilo. Hata hivyo Kanisa hilo halitabomolewa lakini litatuzwa kama ssehemu ya historia ya Ukristu katika eneo hilo.

Kiasi cha fedha kinachohitajika kinapatikana kwa njia za michango na harambee ya waamini.

Akizungmza na gazeti mahalian a New Times, Askofu Alexis Bilindabagabo wa Jimbo la Gahini , ambaye huwakilisha viongozi wa kanisa katika Kamati kuu anasema Kanisa jipya, historia ya Kanisa itarithishwa kizazi hadi kizazi. Na amewahiza waamini katika jimbo hilo kujitolea kwa moyo wa ukarimu zaidi, kufanikisha miapngo ya ujenzi wa kanisa jipya kama inavyotarajiwa.








All the contents on this site are copyrighted ©.