2013-09-03 09:00:41

Shule ya Ratzinger- Mahali pema ni karibu na Kristu.


Wanadamu huingia kwenye njia ya kweli na haki pale wanapojitahidi kujishusha kwa ajili ya huduma kwa wengine na kusambaza mapendo yake mwenyezi Mungu. Kwa kifupi ndiyo maneno yake Baba Mtakatifu Mstaafu Benedicto wa kumi na sita siku ya Jumapili (01.09.13) pale alipokutana na kuadhimisha ibada ya Misa Takatifu akiwa na wanafunzi wake wa zamani, mjini vaticani.

Hii ilikuwa ni katika harakati za kuhitimisha semina ya wakati wa kiangazi, inayofanywa kila mwaka na wanafunzi wa zamani wa Papa Benedikti XV1, Seminar hii inayojulikana kama Shule ya Joseph Ratzinger.

Mafunzo hayo yamefanyika mjini castelgandolfo chini ya mada: Swala la Mungu katika dunia ya utandawazi (secolarization) kwa mwanga wa mawazo ya falsafa na teologia ya Remi Brague, mwana teoria aliyetunukiwa tuzo la kiteologia la Ratzinger hapo mwaka 2012.

Kwenye mahubiri yake Papa Mstaafu amegusia yale yaliyoongelewa kwenye Injili ya siku ya Jumapili ambapo Yesu anawaalika wafuasi wake kuchukua nafasi ya mwisho kwani nafasi ambazo huonekana njema kwenye macho ya binadamu hudanganya japo watu wengi wanazitafuta sana nafasi hizo kama ilivyojidhihirisha hata kwenye karamu ya mwisho kati ya Yesu na wanafunzi wake. Wanafunzi waligombania nafasi ya kwanza!

Badala yake, Yesu alijionyesha kama mtumishi. Yeye aliyezaliwa kwenye hori la wanyama, anakufa juu ya mti wa msalaba. Yeye aliye Kristo, Mwana wa Mungu, anaonyesha upendeleo kwa maskini na wale wanaosukumizwa pembezoni mwa jamii, anawainua kwa mapendo makuu.

Hivyo baba Mtakatifu Mstaafu ameendesha kweli Katekisimu juu ya umaana wa kushushwa kwa Kristo kwa maana ya upendo. Msalaba ulikuwa mahali pa chini sana, sio hata mahali, ila Kristo alikufa msalabani, kuonyesha hakuwa hata na nafasi yake kwenye jamii; alishushwa haswa. Hata hivyo ni kwa kushushwa huku ambapo Mungu aliwadhimisha mno, akawa wokovu kwa wote waliomlilia. Akala na wenye ukoma na waliopooza. Akawahurumia wote hata akawasamehe na watesi wake, na kutufundisha kwamba hakuna jamii inayoweza kuendelea kukua bila mapendo na msamaha.

Kwa maneno hayo Baba Mtakatifu Mstaafu anatukumbusha na kutualika kuingia kwenye mwuungano wa liturjia ya Kikristo yenye chimbuko lake kwenye Ekaristi takatifu. Mwuungano hasa na Mungu Mwenyewe.








All the contents on this site are copyrighted ©.