2013-09-03 09:10:40

Fungeni na kusali kwa ajili ya amani


Kardinali Oscar Andrès Rodriguez Maradiaga, Rais wa Shirikisho la Mashirika ya Misaada ya Kanisa Katoliki Kimataifa, Caritas Internationalis, atazuru Kanisa la Canada wakati wa Mkutano Mkuu wa Baraza la Maaskofu wa nchi hiyo utakaofanyika kuanzia tarehe 23 hadi 27, Septemba 2013.

Kardinali huyo kutoka Honduras ni mmoja wa washauri 8 walioteuliwa na Baba Mtakatifu Francisko kwa ajili ya mageuzi nchini Vatican atahutubia mkutano huo juu ya mada ya Jukumu la Maaskofu katika kuendeleza haki, amani na mapendo.

Nao Maaskofu wa Canada watachukua fursa hiyo kuchambua kwa kina miaka 50 tangu Baba Mtakatifu Yohane wa 23 alipochapisha hati ya kichungaji Pacem in Terris – Amani Duniani mnamo mwaka 1963 kama moja ya mapendekezo ya mababa wa Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatikani. Mama Kanisa anapoendelea kuadhimisha Kumbu kumbu ya Miaka 50 tangu Mwenyeheri Yohane XXIII alipochapisha Waraka huo wa kichungaji, Pacem in Terris, Amani Duniani, ni changamoto kwa wote kuendelea kuithamini amani kama tunu inayowaunganisha wanadamu wote.

Kardinali Maradiaga pamoja na Maaskofu wa Canada watatumia pia mkutano wa tarehe 23 hadi 27 Septemba 2013 kama wakati muafaka kwa kutafakari juu ya changamoto na mabadiliko ya uongozi wa kanisa nchini humo.










All the contents on this site are copyrighted ©.