2013-09-02 15:12:47

UNESCO- kusaidia ukarabati wa makanisa na Misikiti -Misri


Shirika la Umoja wa Mataifa kwa ajii ya elimu, sayansi na utamaduni( UNESCO), alituma watalaam wake Misri, ili wasaidie kukarabati majengo ya thamani kubwa kihistoria yaliyoharibiwa yakiwemo , Makanisa na Misikiti. Hili limeelezwa na Mohamed Sameh , Balozi wa UNESCO, Misri.

Sameh , Mjumbe wa UNESCO wa kudumu Misri, ameendelea kufafanua kwamba , watalaam kutoka UNESCO, watafanyakazi kwa kushirikiana na Wizara ya mambo ya kale ya MIsri, wakianza na kazi ya kutathimini ukubwa wa kazi na idadi ya makanisa, Miskiti, monesteri na majengo mengine ya kihistoria, likiwemo jengo la makumbusho la Mallawi , na kiassi cha fedha kitakachohitajika katika kazi hizo za ukarabati.

Aidha inaelezwa kwamba hivi karibuni kutafanyika warsha katika makao makuu ya UNESCO, Mjini Nairobi Kenya , juu ya ulinzi na ukarabati wa urithi wa kihistoria wa Misri.

Wamisri huonea fahari historia yao iliyoanza hata kabla na baada na Yesu kuzaliwa,kama inavyoelezwa katika Injili ya Matayo, familia ya Yesu ilikimbilia Misri wakati wa madhulumu makali ya Mfalme Herode. Na Kanisa la Kikoputiki Misri , hujivunia historia kwamba Mtume Marko, mfuasi wa Yesu na Mwinjilisti, aliinjilisha katika mji wa Alexandria kabla kuuawa kwake na wapinzani wa Ukristu.

Hivyo Misri ni chungu cha historia, tangu zama za kale. Kuna majengo mengi yanayoelezea historia, yanayoheshimiwa na UNESCO, kama hazina na urithi mkubwa wa dunia.

Mwanahistoria Meinardus ameandika juu ya ukuu na utajiri wa Historia ya Ukristu Misri, katika muono wa uwepo wa idadi kubwa ya watu mashuhuri katika Ukristu kufika misri, kama Wataktifu Athanasius, Cyril, Pachomius....
.
Na ingawa leo hii , Wakristu ni kati ya makundi madogo ya imani katika eneo la Mashariki ya Kati na Kaskazini mwa Afrika, wakiwa katika kiwango cha asilimia kati ya 10-15 nchini Misri, katika miaka ya mwanzo ya AD, ukristu ulishamiri hadi dini mpya zilipoingia ukiwemo Uislamu, ambao leo hii, unaongozwa kwa kuwa na idadi kubwa ya wafuasi Misri.

Upande wa Wakristu , idadi kubwa ni Waotodosi wa Kanisa la Kikoptiki , na pia kuna idadi dogodogo za waamini wa makanisa Katoliki, Protestanti na makanisa ya Mashariki. Yote hayo yana historia ya kuvutia katika taifa hilo la Misri.








All the contents on this site are copyrighted ©.