Jumuiya ya kimataifa yahimizwa kutokalia kimya kilio cha wahanga wa vita Syria
Kwa mara ingine Jumuiya ya kimataifa imehimiza kukisikia kilio cha wahanga wa vita
Syria. Ni wito uliotolewa na Askofu Mkuu Mario Zenari, Mjumbe wa Papa Syria AskofuMkuu
Mario Zenari, ametoa himizo hili, kwa kurejea ombi lililotolewa na Papa Francisko,
Jumapili iliyopita ambamo aliitaka Jumuiua ya Kimataifa kufanya kila linalowezekana
kuisaidia Syria kupata jibu linalofaa kusitisha mzozo wa kisiasa unaoendelea. Askofu
Mkuu Mario anasema, jumuiya ya Kimatiafa inao wajibu wa kutoa jibu katika kipeo hicho,
ambacho mpaka sasa kimegharimu maisha ya maelfu ya watu wasiokuw na hatia . Inasikitisha
sana kuoana picha zilizo tolewa na kukisikia kilio cha wadogo wasiokuwa na hatia .
Hivyo si haki kwa jumuiya ya kimataifa kujifanya haioni mateso na mahangaiko ya watu
wa Syria. Askofu Mkuu Zenari anasema anatolea sala zake kwa wote wale wenye
kuwa na mamlaka katika uwanja wa huu wa kimataifa, na viongozi wote katika ngazi
hii ya kimataifa , kutumia busara na hekima kupata jawabu la haraka kukomesha kipeo
cha machafuko Syria, kama Papa Francisko alivyotoa ombi lake wakati wa sala ya Malaika
wa Bwana, Jumapili iliyopita.