2013-08-27 10:21:17

Wabunge Wakatoliki kukutana na Papa Francisko mjini Vatican


Wabunge Wakatoliki kutoka Kenya wako mjini Roma nchini italia kwa madhumuni ya kuhudhuria warsha ya kimataifa kwa ajili ya Wabunge Wakatoliki. Habari iliyochapishwa kwenye jarida la Star la Kenya inasema kwamba, madhumuni ya mkutano huo mjini Roma ni kutafakari na kupanga mikakati ili kuhakikisha siasa zinaoana na mpango wa Mungu kwa watu wake.
Katika mahojiano na jarida la The Star, Makamu Mwenyekiti wa Wabunge wakatoliki nchini Kenya, Bwana Chris Wamalwa, anasema kwamba wakiwa mjini Roma watamtembelea pia Baba Mtakatifu Francisko kwenye Ikulu ya Vatican. Wabunge hao watapata fursa ya kukutana na kujadiliana na wenzao kutoka sehemu mbalimbali za dunia.
Bwana Chris Wamalwa amechukua uongozi wa kundi la wabunge wakatoliki nchini Kenya hivi karibuni kutoka kwa aliyekuwa makamu wa kundi hilo, John Mututho.








All the contents on this site are copyrighted ©.