Ujumbe wa Papa katika Sura ya Nne ya mwanga wa Imani
Monsinyori John Kennedy, Afisa katika Shirika la Kipapa kwa ajili ya Mafundisho Sadikifu
ya Kanisa, akiitafakari sura ya mwisho ya waraka wa Mwanga wa Imani , uliotolewa na
Papa Francisko, amesema sura hii imejikita zaidi katika Barua kwa Waebrania, ambamo
mnaelezwa jinsi Mungu, alivyowaandalia wana wa Isreal, mji kwa ajili yao. Na hivyo
ni habari njema kwa watu wote. Mons. Kennedy anasema, Papa Francisko akiwarejea
Wakuu wa Makanisa na haki za wake kwa waume wa wakati wa Agano la Kale, anaitaja barua
kwa Waebrania, kwamba, ina vigezo maalum katika imani, kwamba, imani si tu huwasilishwa
kama njia, lakini pia kama utaratibu wa kujenga, ambao daima huanza na maandalizi
ya mahali ambamo binadamu anaweza kuishi kwa ushirikiano na wengine. Na mfano
umetolewa kama Noah alivyoandaa safina kwa ajili ya kuiokoa familia yake. Na Abraham
alivyoandaa kuishi katika mahema, wakati akisubiri kwenda katika nchi ya ahadi kwa
matumaini makubwa. Kwa muono huo, Monsinyori Kennedy anaendelea kusema, Papa Francisko
katika sura hii, pia anaonyesha kwamba, uthabiti katika imani, huweka alama za maandalizi
ya kuelekea katika mji wa ahadi unaoandaliwa na Mungu kwa binadamu. Na kwa kutambua
hili, tunaweza kuona kwamba, kwa kila binadamu , imani humwangazia binadamu juu ya
mahusiano yake na Mungu. Na ndani mwake huzaliwa upendo na tafakari zaidi za kuuona
upendo huo wa Mungu mwenyewe. Mungu mwenyewe amini, anaye wapatia waamini wake mji,
mji wa matumaini, usiokuwa na miisho.
Mons Kennedy, anaendelea kuangalisha
katika maisha ya kila siku na matokeo yake anasema, hili ni dhahiri, kama alivyosema
Papa Francisko kwamba, mwanga wa imani , unadai kuwekwa katika huduma ya sheria ya
haki, na amani, mwanga huo unakuwa ni uwezo unaoongeza nguvu katika mahusiano ya binadamu,
na katika kuboresha maisha ya pamoja na mshikamano wa kijamii.
Imani inafanya
sisi kufahamu usanifu wa mahusiano kati ya binadamu kwa sababu imani huzingatia msingi
ya adilifu katika muono wa sheria za Mungu. Na hivyo imani inakuwa huduma kwa manufaa
ya wote.
Papa Francis kisha anasema, imani si tu huangazia a mambo ya ndani
ya Kanisa, au kutumika tu katika kujenga mji wa milele, lakini pia husaidia kujenga
jamii yetu katika njia ya uhakika kwa jamii, kutembea vyema kuelekea mustakabali
wa maisha yenye matumaini.
Anaendelea kuangalisha katika manufaa ya familia
na jamii , kwamba, kuirejesha imani katika familia, inakuwa ni uwasilishaji wa uwezo
wa mwanga, wenye kumulikia mahusiano katika jamii nzima. Ni kuiwezesha familia na
jamii kufanya majiundo adilifu na manufaa ya wote. Huanzia katika jamii kutembea katika
njia ya udugu, kwenye muono kwamba, sisi sote ni wana wa Baba Mmoja wa mbinguni.