2013-08-27 12:31:22

Serikali kufanya sensa ya madhehebu mapya!


Serikali ya Equitorial Guinea imeamua kuendesha sensa ya madhehebu mapya ya Kikristo yaliyoenea nchini humo yanayojulikana kama Makanisa ya Mwamko Mpya. Shirika la habari la Afrika, APA linasema kwamba Wizara ya Haki ya nchi hiyo ya Equatorial Guinea imeunda kamati ambayo tayari imeanza utafiti wa kitaifa kuhusiana na madhehebu hayo mapya.
Lengo la zoezi hilo la Sensa ni kutaka kufahamu kwa kina mwamko huo mpya hasa kulingana na masuala ya haki na sheria. Utafiti huo unafuatia malalamiko kutoka kwa baadhi ya washiriki wake kutokana na kile wanachokiita ufisadi na ulaghai unaoendelea katika baadhi ya Makanisa hayo ambayo yanasemekana yanakusanya fedha kwa malengo ya kujenga Makanisa au shule, lakini hayatimizi malengo hayo.
Nchi nyingi za Kiafrika sasa zinashuhudia kuongezeka kwa madhehebu ambayo yanawavutia watu wengi sana, wengi wakiwa ni wanawake, anasema mwana sayansi jamii mmoja aliyehojiwa na Shirika la habari la APA. Mengi ya makanisa hayo yanaongozwa na Kakasisi kutoka nchi za Nigeria, Cameroon, Ghana na Jamhuri ya Kidemocrasia ya watu wa Congo(DRC).








All the contents on this site are copyrighted ©.