Kanisa linafuatlia machafuko ya kisiasa nchini Misri kwa uchungu na matumaini!
Patriaki Ibrahim Isaac, Rais wa Baraza la Mapatriaki na Maaskofu nchini Misri anasema
kwamba, Kanisa linaendelea kufuatilia matukio ya kigaidi, mauaji ya watu wasiokuwa
na hatia na uharibifu wa miundo mbinu kwa uchungu mkubwa na matumaini kwamba iko siku,
utawala wa sheria utaweza kushika hatamu na amani kutawala tena nchini Misri.
Kanisa
linaunga mkono juhudi zote zinazofanywa na vikosi vya ulinzi na usalama kwa ajili
ya masilahi ya taifa na kwamba, wasingependa kuona watu wanaingilia masuala ya ndani
ya Misri. Wanavishukuru vyombo vya habari vya kitaifa na kimataifa vinavyotekeleza
dhamana yake kwa kuzingatia kanuni, maadili na sheria za kazi, ili kubainisha ukweli
wa mambo.
Kanisa linawashukuru waamini wa dini ya Kiislam waliojitoa mhanga
kwa ajili ya kulinda na kutetea maisha ya viongozi wa Kanisa na Makanisa yaliyokuwa
hatarini kuchomwa moto.
Viongozi wa Kanisa wanapenda kuwajulisha walimwengu
kwamba, kuna mapambano dhidi ya vitendo vya kigaidi nchini Misri na wala hii si vita
ya kidini kama wengi ambavyo wanapendwa kusadikishwa. Wanatuma salam za rambi rambi
kwa wote walioguswa na machafuko ya kisiasa nchini Msiri.