2013-08-20 07:44:20

Salam za rambi rambi kwa Kardinali Sodano


Baba Mtakatifu Francisko ametuma salam za rambi rambi kwa Kardinali Angelo Sodano, Dekano wa Makardinali na familia yake kutokana na kifo cha Mama Assunta Sodano dada yake Kardinali Sodano, kilichotokea hapo tarehe 18 Agosti 2013 na mazishi yanafanyika tarehe 20 Agosti 2013.

Baba Mtakatifu anapenda kumhakikishia Kardinali Sodano na Familia yake uwepo wake wa karibu kiroho wakati huu wanapoomboleza msiba wa dada yao mpendwa. Anaiombea roho ya marehemu Mama Asunta Sodano raha na mwanga wa milele ili uweze kuiangazia, ili aweze kupumzika kwa amani. Anawaomba wote walioguswa na msiba huu kuupokea kwa imani na matumaini ya Kikristo. Mwishoni, Baba Mtakatifu anawapatia baraka zake za kitume wote wanaoshiriki katika msiba huu.

Viongozi mbali mbali kutoka Vatican wametuma pia salam za rambi rambi kwa Kardinali Angelo Sodano, Dekano wa Makardinali kutokana na msiba wa dada yake Assunta Sodano, ambaye aliyatoa maisha yake kwa ajili ya huduma kwa familia na Jumuiya iliyokuwa inamzunguka kama mwalimu na katekista Parokiani kwake, utume ambao aliufanya kwa moyo mkuu.







All the contents on this site are copyrighted ©.