Mshikamano na wakimbizi kutoka sehemu mbali mbali za dunia!
Baraza la Maaskofu Katoliki Hispania linaadhimisha Juma la 41 la Wakimbizi na Wahamiaji,
ili kutoa msukumo wa pekee kwa Jamii kuangalia na kuguswa na mahangaiko ya wakimbizi
na wahamiaji wanaotafuta hifadhi ya maisha Barani Ulaya.
Mahujaji wa Kihispania
kutoka sehemu mbali mbali za dunia, kuanzia tarehe11 hadi tarehe 18 Agosti 2013 wanashiriki
katika hija ya imani kwenye Madhabahu ya Bikira Maria wa Fatima. Kuna idadi kubwa
ya wananchi wa Hispania ambao wamehama au kuikimbia nchi yao kutokana na athari za
myumbo wa uchumi kimataifa. Hili ni kundi ambalo linahitaji kupatiwa msaada na huduma
za kichungaji huko liliko!
Hii pia ni changamoto kwa waamini na wananchi wa
Hispania katika ujumla wao, kuonesha moyo na mshikamano wa dhati kwa wakimbizi na
wahamiaji kutoka sehemu mbali mbali za dunia; watu wanaotaka kusalimisha maisha yao
kutokana na vita, kinzani na hali ngumu ya maisha.