2013-08-10 09:36:56

Baa la njaa linatishia maisha Namibia!


Serikali ya Namibia inasema kwamba, wananchi wake zaidi ya laki nne wanakabiliana na baa la njaa kutokana na ukame wa muda mrefu. Namibia inakadiriwa kuwa na watu zaidi ya millioni mbili. Hali ya sasa ni kama ile iliyojitokeza kunako mwaka 1980, wananchi wengi wa Namibia walipoteseka kwa baa la njaa.

Serikali ya Namibia inaiomba Jumuiya ya Kimataifa kusaidia kuokoa maisha ya wananchi wake wanaokabiliwa na ukosefu wa chakula kwa sasa. Ukame wa muda mrefu una madhara makubwa kwa maisha na maendeleo ya wananchi wa Namibia, lakini waathirika wakubwa ni wale wanaoishi vijijini. Ukame unatishia pia sekta ya utalii ambayo ni chanzo kikuu cha pato la taifa nchini humo. Ukame unaendelea pia kutishia maisha ya wananchi wa Angola.







All the contents on this site are copyrighted ©.