2013-08-09 11:35:16

Jeshi la Polisi Uganda lasikitishwa na wezi wanaomwibia hata Mungu!


Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi nchini Uganda Kale Kayihura amesema amepokea taarifa kutoka Jeshi la Polisi mjini Vatican ikimwomba kufanya uchunguzi wa kina kwa watu wanaotuhumiwa kuiba fedha kutoka Benki ya Vatican na kuziwekeza nchini Uganda.

Jenerali Kayihura ameyasema hayo hivi karibuni alipokuwa anafungua mkutano wa siku tatu wa wakuu wa Jeshi la Polisi kutoka Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika, mkutano ambao umezishirikisha nchi 25.

Anasema, inasikitisha kuona watu wanamwibia Mwenyezi Mungu? Vatican kwa sasa inaendelea kuboresha sheria na mikakati ya kupambana na utakatishaji wa fedha haramu kama njia ya kusimamia misingi ya ukweli, uwazi, uadilifu na uwajibikaji.

Wakati huo huo, habari kutoka Kampala Uganda zinasema kwamba, Jeshi la Polisi nchini Uganda, linamshikilia Esther Nabasa kwa shutuma za kujipatia kiasi cha Euro 287, 180, 000 sawa na shilingi Billioni 1 za Uganda.







All the contents on this site are copyrighted ©.