2013-08-08 12:23:16

Bado watu wanaendelea kumwombea Mzee Madiba


Viongozi mbalimbali wa kidini siku ya Jumatano, tarehe 7 Agosti 2013 waliongoza Ibada ya sala mbele ya Hospitali ambapo amekuwa akiuguzwa kwa miezi miwili sasa aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini, Mzee Nelson Mandela.
Askofu mkuu Joe Seoka wa Jimbo kuu la Preitoria, Kanisa Anglikani alitumia muda huo kuwaomba wananchi wa Afrika Kusini kuendelea kumuombea Mzee Mandela ambaye amekuwa akitibiwa ugonjwa wa mapafu tangu tarehe 8 Juni, 2013, kwenye Hospitali ya Mediclinic iliyoko mjini Pretoria.
Kwa miezi hii miwili Afrika Kusini, familia, ndugu, jamaa na marafiki pamoja na watu wenye mapenzi mema duniani kote, wamekuwa wakimwombea na kumpelekea salamu za matashi mema Mzee Madiba, aliyewahi kupata tuzo ya amani duniani.
Askofu mkuu Seoka anasema kwamba Mwenyezi Mungu anamtumia “Mzee Madiba” na ugonjwa wake kama changamoto kwa wananchi wote wa Afrika Kusini kuweza kuungana na kuyashikilia maadili ambayo aliyapigania Rais huyo wa zamani. Nelson Mandela alitimiza miaka 95 akiwa hospitalini humo tarehe 18 Julai 2013.








All the contents on this site are copyrighted ©.