2013-08-03 12:03:09

Papa Francisko afanya uteuzi kwa ajili ya Tume ya Kipapa ya Kanisa la Mungu na Mtunzaji mkuu wa Sadaka ya Papa


Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Guido Pozzo kuwa Katibu mkuu mpya wa Tume ya Kipapa ya Kanisa la Mungu, Ecclesia Dei. Hadi uteuzi huu, Askofu mkuu Guido Pozzo alikuwa ni mtunzaji mkuu wa Sadaka ya Papa.

Wakati huo huo, Baba Mtakatifu Francisko amemteua Monsinyo Konrad Krajewski, kuwa Mtunzaji mkuu wa Sadaka ya Papa. Hadi uteuzi huu, Monsinyo Konrad Krajewski alikuwa ni Mshereheshaji na Afisa wa Ibada za Kipapa mjini Vatican. Baba Mtakatifu amempandisha hadhi na kuwa ni Askofu mkuu.







All the contents on this site are copyrighted ©.