2013-08-01 08:29:08

Wafanyakazi wa sekta ya afya Kenya kulipwa kwa wakati!


Waziri wa Afya nchini Kenya, James Macharia amesema kwamba wauguzi watalipwa mishahara yao kama ilivyopangwa ili kuzuia mgomo wa madaktari. Waziri amesema kwamba serikali inajali maslahi ya wafanyakazi wa sekta ya afya kwani bila kufanya hivyo watu wengi wanaweza kuathirika na madaktari hao hawatakuwa na uwezo mzuri wa kuwauguza wagonjwa.
Madaktari nchini Kenya walitishia kugoma ifikapo tarehe 4, Agosti 2013 ikiwa serikali haitawapatia mishahara yao ya mwezi Julai. Kawaida mishahara hiyo hulipwa kila tarehe 25 ya mwezi. Kupitia chama chao cha madaktari na wauguzi wa meno, wafanyakazi hao wamesema hawaelewi ni kwa nini mishahara yao inacheleweshwa na Serikali.








All the contents on this site are copyrighted ©.