2013-07-30 06:59:55

Watu 38 wapoteza maisha katika ajali mbaya ya Bus, Italia


Baba Mtakatifu Francisko ametuma salam za rambi rambi kutokana na ajali ya Bus iliyotokea kwenye barabara kuu ya A16 kati ya Napoli-Canosa iliyosababisha watu 38 kupoteza maisha na wengine wengi kubaki majeruhi.

Baba Mtakatifu katika ujumbe ulioandikwa kwa niaba yake na Kardinali Tarcisio Bertone, Katibu mkuu wa Vatican kwenda kwa Kardinali Crescenzio Sepe, Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Napoli anasema, anaungana na wote wanaoomboleza vifo vya ndugu na jamaa zao, anawaombea wote waliopatwa na majeraha kupona haraka.

Serikali ya Italia imetangaza Jumanne tarehe 30 Julai 2013 kuwa ni Siku ya Maombolezo Kitaifa.









All the contents on this site are copyrighted ©.