Vatican na Italia kuendelea kushirikiana katika mapambano dhidi ya utakatishaji wa
fedha haramu!
Mamlaka ya Habari za Fedha Vatican (AIF) tarehe 26 Julai 2013, imetiliana sahihi mkataba
wa makubaliano na Mamlaka ya Habari za Fedha Italia (UIF) kutoka Benki kuu ya Italia.
Kardinali Attilio Nicora, Rais wa AIF ameweka sahihi kwa niaba ya Vatican na kwa upande
wa Italia, sahihi imewekwa na Dr. Claudio Clemente, mkurugenzi mkuu wa UIF.
Makubaliano
haya ni jitihada za Vatican kwa kushirikiana na Serikali ya Italia kuongeza nguvu
katika kupambana na utakatishaji wa fedha chafu katika nchi hizi mbili. Makubaliano
haya yanatoa fursa kwa Serikali ya Italia na Vatican kushirikishana habari kuhusu
fedha pamoja na kutunza siri. Vatican inaendelea kuimarisha juhudi zake za kupambana
na utakatishaji wa fedha chafu pamoja na kugharimia vitendo vya kigaidi.
Kitengo
cha kupambana na utakatishaji wa fedha chafu mjini Vatican kiliundwa hapo tarehe 30
Desemba 2010.