Pokeeni zawadi ya maisha kwa moyo wa shukrani na mapendo!
Baba Mtakatifu Francisko, Jumamosi mara baada ya maadhimisho ya Ibada ya Misa Takatifu
kwa Makleri na Watawa, wakati akitoka Kanisani alikutana na Familia moja iliyokuwa
imebeba mtoto ambaye alizaliwa bila ubongo, watoto ambao mara nyingi hufariki dunia
maramoja! Wazazi hawa kwa utashi wao wenyewe wameamua kuipokea zawadi ya maisha, kuitunza
na kuiendeleza hadi pale Mwenyezi Mungu atakavyo amua mwenyewe.
Padre Federico
Lombardi anasema, tukio hili limemgusa kwa namna ya pekee Baba Mtakatifu Francisko
kiasi kwamba, wazazi na mtoto wao wamealikwa kushiriki katika matoleo na Baba Mtakatifu
mwenyewe amempokea mtoto huyu mikononi mwake wakati wa matoleo, changamoto kwa waamini
na watu wenye mapenzi mema kupokea na kuitunza zawadi ya maisha kutoka kwa Mwenyezi
Mungu.