2013-07-29 11:15:03

Kanisa kuu la Mtakatifu Anna, Brazzaville linaadhimisha Miaka 70 tangu lilipojengwa


Katika Maadhimisho ya Watakatifu Joakim na Anna Wazazi wake Bikira Maria, hapo tarehe 26 Julai 2013, Kanisa kuu la Mtakatifu Anna, Jimbo kuu la Brazzaville, nchini Congo, limeadhimisha Kumbu kumbu ya miaka 70 tangu lilipojengwa. Wakristo na watu wenye mapenzi mema wamesherehekea miaka 70 ya Kanisa kuu la Mtakatifu Anna kwa njia ya: sala, semina, michezo na tamasha la muziki wa dini.

Kanisa kuu la Mtakatifu Anna limo kwenye orodha ya urithi wa binadamu. Ujenzi wa Kanisa ulichangiwa na Mfalme Mohamed wa Morocco na kutoka Ethiopia.







All the contents on this site are copyrighted ©.