Askofu mkuu Tonyè Bakot wa Jimbo kuu la Yaounde, Cameroon ang'atuka kutoka madarakani
Baba Mtakatifu Francisko amekubali ombi la Askofu mkuu Simon Victor Tonyè Bakot wa
Jimbo kuu la Yaounde, Cameroon la kung'atuka kutoka madarakani kadiri ya sheria za
Kanisa namba 401, kipengele 2 na badala yake Baba Mtakatifu amemteua Askofu Jean Mbarga
wa Jimbo Katoliki la Ebolowa kuwa ni msimamizi wa kitume wa Jimbo kuu la Yaounde,
Cameroon.