2013-07-26 11:07:41

Njia ya Msalaba, Kesha na Misa ya kufunga Siku ya 28 ya Vijana Duniani kufanyika kwenye ufuko wa Copacabana!


Kutokana na mvua kuendelea kunyeesha mjini Rio de Janeiro na hivyo kusababisha matope na unyevunyevu mkubwa, Kamati kuu ya Maadhimisho ya Siku ya 28 ya Vijana Duniani kwa Mwaka 2013 imeamua kwamba, Kesha na Misa ya kufunga Siku ya Vijana Duniani, kufanyika kwenye ufuko wa Copacabana badala ya kufanyika kwenye Uwanda wa Guaratiba, kama ilivyokuwa imepangwa hapo awali. Uwanda huu ulikuwa umepachikwa jina, "Campus Fidei" yaani Uwanda wa Imani. RealAudioMP3

Ufuko wa Copacabana ni mahali ambapo Ibada ya Misa takatifu kwa ajili ya ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani imefanyika, kwa kuongozwa na Askofu mkuu Joao Tempesta. Hapa vijana wanafanya Njia ya Msalaba na kwamba, matukio ya mwisho yanatarajiwa kuhudhuriwa na vijana zaidi ya millioni mbili na nusu. Mabadiliko haya yamesababisha usumbufu mkubwa, lakini yote ni kwa ajili ya mafao na ustawi wa vijana.







All the contents on this site are copyrighted ©.