2013-07-25 08:22:15

Maadhimisho ya Siku za Vijana Duniani yamekuwa ni chemchemi ya miito ndani ya Kanisa!


Baba Mtakatifu Francisko anamshukuru kwa namna ya pekee Mwenyeheri Yohane Paulo wa pili ambaye alibuni na kuanzisha Maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani ambayo kwa Mwaka huu yamefikia awamu ya Ishirini na nane.

Siku za Vijana Duniani anasema Baba Mtakatifu Francisko zimekuwa ni chemchemi ya miito mbali mbali ndani ya Kanisa. Hii ni sehemu ya ujumbe wa Baba Mtakatifu kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii.

Itakumbukwa kwamba, katika Maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani, onesho la miito mbali mbali ndani ya Kanisa limekuwa ni kivutio kikubwa kwani hapa Mashirika mbali mbali ya kitawa na kazi za kitume yanajinadi mbele ya vijana, yakijitahidi kuwachangamotisha ili kujitosa kimaso maso kumfuasa Kristo kwa njia ya maisha ya Kipadre na Kitawa.

Katika Maadhimisho ya Mwaka huu, Onesho la Miito mitakatifu ndani ya Kanisa linafanyika kwenye Uwanja wa Quinta da Boa, hapa kuna zaidi ya Mashirika ya Kitawa na Kazi za kitume yenye mwelekeo wa kimataifa zaidi ya mia moja yanayoendelea kujinadi na kuna umati mkubwa wa vijana wanaopita na kuangalia wapi ambapo Roho wa Bwana ataweza kuwatuma.







All the contents on this site are copyrighted ©.