2013-07-23 09:57:20

Baada ya safari ndefu, Baba Mtakatifu anavuta kasi!


Jumanne, tarehe 23 Julai 2013 baada ya safari ndefu, atapata mapumziko mafupi kwenye makazi ya Sumarè, mjini Rio de Janeiro.

Jumatano, tarehe 24 Julai 2013 itakuwa ni siku maalum kabisa ambayo Baba Mtakatifu Francisko ataitumia kwa ajili ya kufanya hija ya maisha ya kiroho kwa Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili wa Aparecida. Hapa ataadhimisha Ibada ya Misa Takatifu.

Baadaye mchana, Baba Mtakatifu Francisko na msafara wake watapata chakula cha mchana pamoja na Maaskofu na Waseminari kwenye Seminari ya Yesu mchungaji mwema ya Aparecida. Baba Mtakatifu jioni, atatembelea na kufungua Hospitali ya Mtakatifu Francisko inayotoa huduma kwa wagonjwa wa afya ya akili.








All the contents on this site are copyrighted ©.