Salam na matashi mema kutoka kwa Papa Francisko kwa wakuu mbali mbali wa nchi
Baba Mtakatifu Francisko wakati wa safari yake ya kichungaji kuelekea Rio de Janeiro,
Brazil amewaandikia ujumbe marais na wakuu wa nchi mbali mbali ambamo atapita wakati
wa safari yake amewaombea: baraka, amani na utulivu. Katika salam zake kwa Rais Giorgio
Napolitano wa Italia, Baba Mtakatifu anasema, anakwenda Brazil ili kukutana na vijana
kutoka sehemu mbali mbali za dunia, ili aweze kuwaimarisha wawe ni mashahidi wa upendo
na wajenzi wa amani.
Baadhi ya wakuu wa nchi walioandikiwa ujumbe na Baba Mtakatifu
Francisko ni: Italia, Algeria, Mauritania na Senegal.