2013-07-20 13:58:04

Vijana kutoka Uingereza wapo "gado" kumsubiri Papa Francisko!


Ujumbe wa vijana 800 kutoka Uingereza unaoongozwa na Maaskofu 5 umewasili mjini Rio de Janeiro, tayari kushiriki katika Maadhimisho ya Siku ya 28 ya Vijana Duniani kwa mwaka 2013. Baba Mtakatifu Francisko anatarajiwa kuwasili nchini Brazil, jumatatu jioni. Vijana hawa wamejiandaa kiroho na kimwili ili kushiriki katika Maadhimisho haya ambayo ni hija ya maisha ya kiroho.

Taarifa inaonesha kwamba, kuna idadi kubwa pia ya waandishi wa habari kutoka Uingereza wanaoshiriki katika Maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani. Vijana wanaalikwa na Baba Mtakatifu Francisko kuwa ni Wainjilishaji wa vijana wenzao katika mitandao ya kijamii.







All the contents on this site are copyrighted ©.