Baba Mtakatifu Francisko ametuma salam za rambi rambi kwa Jimbo kuu la Bombay, India
kutokana na kifo cha Kardinali Simon Ignatius Pimenta, Askofu mkuu mstaafu wa Jimbo
kuu la Bombay. Baba Mtakatifu anamkumbuka kwa namna ya pekee Marehemu Kardinali Pimenta
kutokana na majitoleo yake kwa Kanisa na uaminifu mkubwa aliouonesha kwa Khalifa wa
Mtakatifu Petro enzi ya uhai wake.
Baba Mtakatifu anaungana na Familia ya
Mungu, Jimbo kuu la Bombay kwa ajili ya kumwombea Marehemu kardinali Pimenta, ili
roho yake iweze kupata pumziko la milele. Baba Mtakatifu anatoa baraka zake za kichungaji
kwa wale wote watakaoshiriki katika Ibada ya Mazishi ya Kardinali Simoni Ignatius
Pimenta.