2013-07-19 14:58:43

WYD 2013 yaiva- Vijana waanza kumiminika Rio de Janeiro.


Vijana kutoka pande mbalibmali za dunia wameanza kumiminika katika mji wa Rio de Janeiro Brazil, kushiriki katika adhimisho la 28 la Siku ya Vijana ya Dunia 2013. Papa Francisko wiki ijayo ataungana na vijana katika sherehe hizo, zinazoanza rasmi tarehe 23 hadi 28. Kati ya mambo mengine muhimu, Papa,ataongoza Ibada za misa, njia ya Msalaba na Mkesha wa sala.
Taarifa tokea Rio zinasema, kwa ajili ya kufanikisha utuaji wa ndege nyingi zinazoelekea Rio de Janeiro, kupeleka maelfu ya mahujaji vijana , utawala umefungua viwanja vingine vinne vya ziada, na kuongeza idadi ya wafanyakazi katika viwanja vya ndege kwa asilimia 58, ili kukabiliana na ongezeko la mahitaji katika viwanja vya ndege, ambako kunatazamiwa zaidi ya vijana 700,000, kuingia Brazil katika kipindi cha wiki moja la maadhimisho ya WYD 2013.
Kardinali Claudio Hummes kutoka Brazil , akilizungumzia tukio hili, amesema ,Papa kushiriki katika maadhimisho haya, kunaonyesha jinsi Kanisa linavyo jali kuwa karibu na watu wahitaji na maskini. Na inatumainiwa muda huu, utakuwa pia ni nafasi nzuri kwa Papa Francisko, kupata picha ya wazi zaidi,katika mwelekeo mpya, unaofaa kwa Kanisa, kulingana na ishara za nyakati , na mikakati mbinu mipya ya kuwa karibu zaidi na watu kwa ajili ya ufanikishaji juhudi za uinjilishaji mpya.
Akiwa Brazil, Papa ana ratiba zito ya kutembelea maeneo mbalimbali hasa yaliyo nje ya jiji la Rio, kama alivyopendekeza Yeye mwenyewe , kukutana na watu wahitaji, zaidi wanaoteswa na hali za umaskini.
Kardinali Hummes, katika mahojiano na Redio Vatican, aliendelea kusema, kwa jinsi mipango na taratibu za Papa zilivyo, zinatoa somo kwetu sote kwamba, si lazima kuwa na mipango mikubwa mikubwa katiak kuwahudumia watu , lakini ni kinacho hitajika zaidi ni kufika kwa watu na kukutana nao katika hali zao za kawaida , kuwa karibu nao na kufanyakazi zao na kuwatia nguvu za kusonga mbele na maisha bila kukata tamaa. Watu hawa wapo mbele ya macho yetu, wakihitaji huduma na kutendewa kwa haki na wakihitaji tabasamu na kumkumbatiwa,kutiwa nguvu na ujasiri mpya kimaisha, kwa mwanga wa huruma na faraja na tumaini Kiinjili.
Kardinali alimalizia maelezo yake kwa kutoa himizo kwa vijana, kusikiliza kwa makini, si tu katika majadiliano na mazungumzo au maadhimisho ya pamoja ya kiliturujia, lakini pia wanahitaji kushiriki kwa dhati katika matukio na madhari zote zitakazotolewa zikiwemo katekesi na vipindi vya maswali na majibu.
Kwa mujibu wa ratiba iliyopo, Papa Francisko ataanza safari kelekea Rio de Janeiro, Jumatatu 22 July tokea uwanja wa ndege wa Fiumicino Roma, na atasafiri na ndege ya Altalia, kwa umbali wa kilomita 9,201 mwendo wa saa 16 hadi uwanja wa ndege wa Rio de Janeiro. Katika uwanja huo, atapokelewa na wenyeji wa Brazil, akiwepo Rais wa Jamhuri ya Brazil, Bi Dilma Rousseff, na ujumbe wake , pia Askofu wa Sao Sebastiao wa Rio de Janeiro, AskofuMkuuu Oran JoaĆ² Tempesta, pia Rais wa Baraza la Maaaskofu Katoliki Brazil, Kardinali Raymond Damasceno Assis na viongozi wa Kiserikali wa Rio de Janeiro.
Uwanjani hapo patafanyika khafla fupi ya Mapokezi kama ilivyoandaliwa katika jengo la Guanabara, na baada ya hapo Papa atakutana kwa faragha na Rais wa Brazil, Bibi Dilma Vana Rousseff. Na mara atasafiri kwa gari umbali wa kilomita 7na nusu hadi katika makazi ya Askofu Mkuu wa Rio de Janeiro, ambako atafikia.








All the contents on this site are copyrighted ©.