2013-07-19 11:26:31

Viongozi wapya wa SECAM


Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Afrika na Madagascar katika mkutano wake mkuu wa kumi na sita uliofunguliwa na Kardinali Polycarp Pengo, Rais wa SECAM aliyemaliza muda wake, umewachagua viongozi wafuatao:

Askofu mkuu Gabriel Mbilingi wa Jimbo kuu la Lubango, Angola, Rais wa SECAM.

Askofu Louis Portella Mbuyu wa Jimbo la Kinkala, Congo Brazzaville, Makamu wa Rais SECAM.

Askofu mkuu Anokye wa Jimbo kuu la Kumasi, Ghana, Makamu wa Pili wa Rais SECAM.

Mheshimiwa Padre Joseph Komakoma kutoka Zambia, Katibu mkuu wa SECAM.

Mheshimiwa Padre Père Samuel de Jesus Paquete, kutoka Angola, Katibu mkuu Mwambata wa SECAM.







All the contents on this site are copyrighted ©.