2013-07-19 10:54:18

Uharamia unaanza kunukia tena Afrika Magharibi!


Vitendo vya uharamia vilivyokuwa vimeanza kutulia kidogo mara baada ya Jumuiya ya Kimataifa kulivalia njuga tatizo hili, vimeanza kujitokeza tena huko Afrika Magharibi.

Hivi karibuni Meli iliyokuwa imebeba shehena ya kemikali ilitekwa nyara na maharamia kutoka Togo, hali ambayo imeanza kutishia usalama wa maisha na bidhaa kwenye Ghuba ya Afrika Magharibi inayoziunganisha nchi za Nigeria, Togo, Ghana na Pwani ya Pembe. Hizi ni nchi ambazo zinasafirisha bidhaa nyingi kwenye soko la kimataifa kwa kupitia mlango wa bahari.

Uharamia umepelekea Makampuni ya Meli kuongeza gharama za bima, hali ambayo imesababisha watu wengi kutowekeza katika sekta ya usafirishaji baharini.







All the contents on this site are copyrighted ©.