2013-07-19 14:48:28

Mkutano Mkuu VII waWasalesiani wa Kujitiolea Wanawake, waanza mjini Roma


Alhamsi Julai 18, majira ya jioni katika Makao Makuu ya shirika la Wasalesiani hapa Roma, kulianza Mkutano wa Mkuu wa VII, wa chama cha watu wa kujitolea wa Don Bosco (VDB), Taasisi ya kidunia ya Wanawake Wasalesian, ambayo ni sehemu ya familia ya kubwa ya Shirika la Wasalesiani.
Mada za mkutano zinazojadiliwa na wajumbe wa VDB wapatao 100, wakiwakilisha kundi kubwa la wanachama 1300, waliotawanyika pande zote za mabara matano ya dunia: ni majiundo ya kudumu katika maisha yaliyowekwa wakfu, katika mtazamo wa aya kutoka Injili ya Yohaneā€¯ Mama unalilia nini? Unatafuta nini? (Yohana 20.15)". Hii ni kauli mbiu iliyochaguliwa kuongoza Mkutano huo, utakaoendelea hadi Jumapili ijayo 28 Julai2013.
Ratiba ya Mkutano huu, ilifunguliwa kwa Ibada ya Misa iliyoongozwa na Gombera Mkuu wa Wasalesiani , Padre Pascual Chavez Villanueva, ambamo pia alitoa hotuba ya ufunguzi. Pamoja na tafakari juu ya mada zilizopendekezwa, Mkutano pia utakuwa na kazi ya kumchagua Mkuu mpya wa VDB, na wajumbe katika Baraza la ushauri kwa wanawake.
Utume wa Wanachama wa Kujitolea wa Don Bosco, daima ni kushuhudia ukweli katika kila mitazamo ya maisha na kila mazingira. Wanawake hawa wa kujitolea, hawaishi maisha ya kujitenga kipweke kama kijumuiya ya watawa , ingawa huziishi nadhiri tatu za Watawa Wasalesiani: usafi wa moyo, umaskini, na utii, katika familia, katika kazi, katika maisha ya kijamii, kisiasa, na katika muungano na mshikamano na parokia, na katika hali zote za kujitolea, katika ulimwengu wa utamaduni na mawasiliano na mitazamo mingine ya maisha adilifu ya kijamii. Kwa lengo hili, VDB, haihesabiki kama ni shirika la maisha yaliyowekwa wakfu, lakini wanachama wake huyaishi maisha hayo, kwa lengo la kufanikisha utendaji ulio bora na fanisi zaidi, hasa, katika mazingira magumu na mipakani.
Chama hiki kilianzishwa mwaka 1917 na Mwenye Heri Padre Philip Rinaldi, akiwa khalifa wa III wa Don Bosco. Wanacahama wake huyaishi maisha ya Kiroho ya Wasalesiani, na kwa namna ya kipekee hutoa angalisho kwa vijana na huyazamisha maisha ya ndani ya kiroho kwa Ibada za Ekaristi na sala kwa Mama Maria.








All the contents on this site are copyrighted ©.