2013-07-18 10:18:36

Simameni kidete kulinda na kutetea haki msingi za binadamu kama njia ya kumuenzi Mzee Madiba


Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Ban Ki-Moon ametuma salam na matashi mema kwa Mzee Nelson Mandela ambaye tarehe 17 Julai 2013 ameadhimisha Miaka 95 tangu alipozaliwa. Maadhimisho haya yanapaswa kuwa ni kikolezo cha ujenzi wa mshikamano na huduma kwa wengine; kwa kusimama kidete kulinda na kutetea haki msingi za binadamu kama alivyofanya Mzee Madiba.

Jumuiya ya Kimataifa anasema Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa inapaswa kutenda sanjari na kuibua mawazo yatakayoleta mabadiliko katika mchakato wa ujenzi wa dunia yenye amani, usawa na maendeleo endelevu kama njia ya kumuenzi Mzee Madiba aliyefanikiwa kumwilisha ndani mwake fadhila mbali mbali za kibinadamu na kiutu.







All the contents on this site are copyrighted ©.