2013-07-17 10:39:03

Umoja wa Ulaya wala Marekani, hawataruhusiwa kuangalia uchaguzi mkuu nchini Zimbabwe!


Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Africa, SADC imewataka wananchi wa Zimbabwe kuonesha utashi na ukomavu wa kisiasa na kidemokrasia katika mchakato mzima wa uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika nchini humo hapo tarehe 31 Julai 2013.

Katika uchaguzi huu, SADC inatarajia kutuma waangalizi wa uchaguzi 442, watakaoangalia mchakato mzima wa uchaguzi katika vituo 210. Umoja wa Afrika kwa upande wake, unatarajia kutuma wajumbe 60. Serikali ya Zimbabwe imesema kwamba, haitawapokea waangalizi wa uchaguzi kutoka Umoja wa Ulaya wala Kituo cha Jim Carter kutoka Marekani, kwani hizi ni nchi ambazo zimeiwekea Zimbabwe vikwazo vya kiuchumi.







All the contents on this site are copyrighted ©.