2013-07-17 12:08:08

Papa: Uhai wa kila binadamu una thamani kubwa isiyokuwa na mbadala


Katika ujumbe wake kwa Wakatoliki wa Ireland, Scotland, Uingereza na Wales, Papa Francesco , amesema, thamani ya uhai wa kila binadamu huanza tangu pale anapotungwa mimba, na hivyo ni lazima kulindwa dhidi ya hali na utendaji wote unaotaka kuyaangamiza bure kama utoaji wa mimba kwa makusundi.

Papa ametoa ujumbe huo kwa ajili ya Siku ya Kitaifa ya kila mwaka kwa ajili ya utetezi wa maisha, ambayo huadhimishwa katika himaya ya Ufalme wa Uingereza kitaifa kwa tarehe iliyochaguliwa kila mwaka kwa kila taifa.

Lengo kuu ni kutoa msisitizo juu ya thamani ya uhai wa binadamu, usiyokuwa na mbadala katika kipimo kwa maisha ya binadamu. Papa anasema katika ujumbe huo, hata binadamu walio dhaifu na wanaokabiliwa na mazingira magumu zaidi, wagonjwa, wazee, na watoto walio bado katika matumbo ya mama zao, uwepo wao wote ni kazi ya thamani sana, ya uumbaji wa Mungu, aliyemfanya binadamu kwa mfano wake. Utendaji unaotoa uhai katika mastahili ya kuheshimiwa daima. Papa ameinua sala zake kwa nia ya kuombea siku hii ili iweze kugusa mioyo ya watu, kuyathamini maisha ya binadamu na kuyatetea katika kila hali hadi katika kifo chake cha kawaida.

Mada inayoongoza adhimisho la mwaka huu ni : Kuyatetea maisha, kuna thamani yake. Ni maneno yaliyochukuliwa kutoka katika mahubiri ya mwaka 2005 ya Kardinali Bergoglio , ambaye sasa ni Papa Francisko, wakati akiongoza Ibada ya Misa kwa heshima ya Mtakatifu Raymondo Nonnato, mlinzi wa wanawake wajawazito. Mtaktifu Raymond Nonnato, alikuwa Mtawa wa Hispania, aliyeishi karne ya kumi na tatu, ambaye, kulingana na simulizi , mama yake alifariki mara baada ya yeye kuzaliwa kwa njia ya upasuaji.

Kama ilivyo kiiini cha Siku hii ya kitaifa kwa ajii ya utetezi wa Maisha ya watu wanyonge, wasiozaliwa bado, wazee na wasiojiweza, wanaoishi ndani ya familia , Maaskofu wanatoa wito kwa watu wote, kuwa na huruma na kukuza huduma kwa watu binadamu hao wanyonge wasioweza kujitetea wenyewe, hasa wanapo pambanisha na hali ngumu za kutaka maisha yao kuangamizwa bure.









All the contents on this site are copyrighted ©.