2013-07-17 08:39:28

"Majembe ya Shirika la Wamissionari wa Damu Azizi ya Yesu kwa Mwaka 2013-2019"


Mheshimiwa Padre Walter Milandu ambaye aliwahi kuwa Gombera wa Seminari kuu ya Shirika la Wamissionari wa Damu Azizi ya Yesu, Vikarieti ya Tanzania na Makamu mkuu wa Shirika Vikarieti ya Tanzania, ni kati ya viongozi wakuu wa Shirika la Wamissionari wa Damu Azizi ya Yesu waliochaguliwa katika mkutano mkuu wa ishirini wa Shirika, unaoendelea mjini Roma. Wengine ni pamoja na:
Mhe. Padre William Nordenbrock, Mkuu wa Shirika la Wamissionari wa Damu Azizi ya Yesu.
Padre Emanuele Lupi, Makamu Mkuu wa Shirika kutoka Kanda ya Italia
Padre Walter Milandu, Mshauri kutoka Vikarieti ya Tanzania.
Padre Henry Brightraj, Mshauri kutoka Vikarieti ya India.
Padre Giandomenico Piepoli, Mshauri kutoka Kanda ya Italia.
Itakumbukwa kwamba, Mheshimiwa Padre Felix Mushobozi kutoka Vikarieti ya Tanzania alikuwa ni Mtanzania na Mwafrika wa kwanza kuchaguliwa kuwa Katibu mkuu wa Shirika katika uongozi uliomaliza muda wake. Mheshimiwa Padre Walter Milandu anakuwa ni Mtanzania wa pili kuchaguliwa katika uongozi wa ngazi ya juu wa Shirika la Wamissionari wa Damu ya Yesu, wakati huu wanapoendelea kujiandaa kwa Maadhimisho ya Miaka 200 tangu lilipoanzishwa, yaani tarehe 15 Agosti 1815.








All the contents on this site are copyrighted ©.