2013-07-16 11:31:05

Madai ya kuwepo hali ya amani na utulivu Afrika ya Kati yapingwa


Kiongozi wa kipindi cha mpito Jamhuri ya Watu wa Afrika ya Kati Bwana Michel Djotodia anasema, hali ya amani na utulivu inaanza kurejea tena kwenye mji mkuu wa Bangui, ingawa wafanyakazi wa Mashirika ya Misaada wanakanusha habari hizi.

Akiwa nchini Burkina Faso Bwana Djotodia amesema kwamba, kikwazo kikubwa kwa amani na usalama nchini mwake ni kutokana na uwepo wa Vikosi vya Jeshi la Waasi kutoka Uganda, LRM, ambalo limekuwa likiendesha mikakati yake nchini humo.

Bwana Djotodia aliingia madarakani mara baada ya vikosi vya Seleka kumwangusha kutoka madarakani Rais Francois Bozize. Watetezi wa haki za binadamu wanasema kwamba, Vikosi vya Seleka vimefanya uharibifu mkubwa kwenye vijijiji mbali mbali tangu Mwezi februari, 2013 na kwamba, Jumuiya ya Kimataifa inaendelea kufumbia macho mateso na mahangaiko ya wananchi wa Jamhuri ya Afrika ya kati, ambao kwa sasa idadi yao inafikia wananchi millioni 4.6. Vikosi cya Seleka vimekuwa vikishutumiwa kwa kujihusisha na vitendo vya ubakaji na nyanyaso za kijinsia,







All the contents on this site are copyrighted ©.