ICC: Rais Uhuru Kenyata na William Ruto kesi yao haiwezi kusikilizwa Kenya!
Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai imetupilia mbali rufaa ya Rais Uhuru Kenyata
na Makamu wake wa Rais William Ruto ya kutaka kesi inayowakabili mahakamani hapo,
isikilizwe nchini Kenya, baada ya kutuhumiwa kujihusisha na machafuko ya kisiasa yaliyoibuka
mara tu baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika kunako mwaka 2007.
Katika machafuko
hayo, watu 1200 walipoteza maisha na wengi kulazimika kuyakimbia makazi yao. Mahakama
ya Kimataifa ilikuwa inaafiki wazo la kusogeza kesi kwa Jumuiya iliyoathirika, lakini
kwa kesi ya Kenya, jambo hili haliwezekani.