2013-07-15 10:09:45

Mzee Madiba bado ngangari!


Mzee Nelsona Mandela ambaye amelazwa Hospitalini kutokana na hali yake kudhohofu, wakati wowote kuanzia sasa anaweza kutolewa Hospitalini na kurudishwa nyumbani ili kuendelea na matibabu akiwa nyumbani kwake.

Hayo yamesemwa na Rais mstaafu Thabo Mbeki wa Afrika ya Kusini, mwishoni mwa Juma, katika hotuba yake kama kumbu kumbu ya mchango wa Mzee Madiba, katika mkutano mkuu wa Chama cha Ukombozi cha Afrika ya Kusini, ANC. Wachunguzi wa mambo wanasema, kwa hakika Mzee Madiba "amekuwa ngangari hata kwa kifo".

Alikaa kifungoni kwa miaka 27 na kunako mwaka 1994 akachaguliwa kuwa Rais wa Afrika ya Kusini na kung'atuka madarakani kunako mwaka 1999. Thabo Mbeki akarithi kigoda cha Mzee Madiba.







All the contents on this site are copyrighted ©.