2013-07-15 08:36:02

Mwaka wa Imani: Wanovisi na walelewa iweni watu wa imani, matumaini na mapendo!


Rev. Dr. Sr. Sabina Patrick Mangi wa Shirika la Masista wa Mtakatifu Theresa wa Mtoto Yesu, Jimbo Katoliki Iringa, ambaye kitaaluma ni daktari wa binadamu, katika Maadhimisho ya Mwaka wa Imani, anawaalika Watawa, lakini Wanovisi na Walelewa kwa namna ya pekee kuhakikisha kwamba, wanakuwa na imani, matumaini na mapendo thabiti kwa Mungu na watu wote ambao Mama Kanisa atawakabidhi ili kuwahudumia. RealAudioMP3

Wanapaswa kuwa na ujasiri katika kumtangaza Yesu Kristo aliyeteswa, akafa na kufufuka kutoka katika wafu, kiini na chemchemi ya imani ya Kanisa. Katika maisha yao, watu wamwone Kristo aliye hai katika nafsi zao.

Anawashukuru na kuendelea kuwaombea wazazi wa watawa, wanovisi na walelewa. Anawahimiza wazazi kutambua na kutekeleza wajibu na dhamana waliyokabidhiwa na Mama Kanisa ya kuhakikisha kwamba, Familia inakuwa ni Kanisa dogo la nyumbani, kitalu cha miito, shule ya utakatifu, haki, amani, upendo na msamaha.

Wazazi wajikite katika kurithisha imani na tunu msingi za maisha ya Kikristo na kiutu zitakazomwilishwa na watawa wakati wa kutekeleza maisha na utume wao ndani ya Kanisa na Jamii kwa ujumla.







All the contents on this site are copyrighted ©.