2013-07-15 14:56:39

Ifungulieni milango ishara ya matumiani na amani - Papa


Papa Francisko , Jumapili mchana , kabla ya sala ya Malaika wa Bwana, alitembelea Makazi madogo ya Kipapa yaliyoko Castel Gandolfo, nje kidogo ya jiji la Roma. . Mahali hapo maelfu ya watu walikusanyika wakiwa wenyeji, mahujaji , wageni na wafanyakazi katika majengo ya Kiapap ya Castel Gandolfo, wakiongozwa na Meya wa mji na Askofu Marcello Seneraro , Askofu wa Albano, kumlaki na kumsikiliza Papa . Papa kwa heshima zote aliwashukuru kwa kufika kumlaki na aliwahimiza wawe macho kuzisoma ishara za matumaini na amani duniani.

Hii ilikuwa ni mara ya pili kwa Papa Francisko, kutembelea Castel Gandofo. Mara ya kwanza, alikwenda katika majengo hayo kumsalimia Papa Mstaafu Benedikto XV1 wakati akiishi katika majengo hayo, mara baada ya kustaafu mwezi March, mwaka huu.
Papa Francisko, akihutubia wakati wa sala ya Malaika wa Bwana, Papa alirejea mfano wa Msamaria Mwema uliotajwa katika somo la Injili ya Jumapili. Na pia alimtaja Mtakatifu Camillo de Lellis, Padre raia wa Italia, Msimamizi na mfariji wa wagonjwa. Mtakatifu Camillo de Lellis alifariki Julai 14 1614, pia ni mwanzilishi wa shirika la Camillian,ambalo utume wake ni kuhudumia wagonjwa na majeruhi katika vita.
Katika hotuba yake, Papa, ilihimiza wote waliokuwa wakimsikiliza, wawe ishara ya matumaini na amani, daima wakijali na kuwa tayari kutoa huduma kwa watu wengine na hasa familia zilizo katika hali ngumu. Alilitaja hili kuwa ni muhimu. Na Wafuasi wa Kristu , ni lazima, wawe ishara ya matumaini na amani kwa wakati huu,ambamo dunia inasongwa na ghasia na machafuko mengi. Wakaristu ni muhimu kuifungua mlango ya matumaini, ili kwamba matumaini yaweze kusonga mbele na kufanikisha amani ya kudumu.

Pia aliwakumbuka watangulizi wake, Mwenye Heri Yohane Paulo II na Mstaafu Papa Benedikto XVI, ambao walipendelea wakati huu wa kiangazi, kwenda kupumzika katika makazi ya Castel Gandolfo ,ingawa waliendeelea kukutana na watu mbalimbali, wakitimiza utume wao wa kuhimiza watu kutembea katika njia nyofu ya Kristu kama Kanisa linavyofundisha.
Papa alionyesha kujali kwamba, wengi wao , wamekuwa na uzoefu wa kukutana nao na kuwakaribisha, katika kipindi hiki . Uzoefu na kumbukumbu hizo na ziwe ushuhuda na faraja, katika uaminifu wa kila siku kwa Kristo na katika juhudi za kuendelea ya kuishi maisha sambamba na mahitaji ya Injili na mafundisho ya Kanisa.
Papa akimgeukia Mtakatifu Camillo de Lellis, alisema, katika kuikumbuka tarehe hii 14 Julai, alimokufa Mtakatifu huyo, inakuwa ni ishara ya kufungua pia sherehe kutimia karne nne za shirika lake au uwepo wa wafuasi wake. Kwa ajili hiyo, Papa kwa namna ya pekee, alitolea sala zake hasa kwa kwa ajili ya Madaktari, Wauguzi na wahudumu wa afya , ambao huendelea kufanya kazi yao bila kuchoka kama ilivyo tajwa katika mfano wa msamaria mwema, katika dunia yetu hii iliyojaa mateso na masumbuko.
Papa pia aliangalisha katika safari yake ya kutembelea Brazil hivi karibuni ambako maelfu ya vijana watakusanyika kutoka pande zote za dunia. Na hivyo , alitolea sala zake kwa ajili ya wote watakaoshiriki katika hija hii hadi Rio de Janeiro , ili kwamba mioyo yao iweze kufunguka katika utume waliofunuliwa na Kristo.
Aidha alisali kwa ajili ya kumbukumbu ya miaka 70 tangu kulipotokea mauaji ya kinyama ya maelfu ya raia wa Poland waliouawa na vikosi vya kijeshi vya Ukraina. Alitoaleaa sala kEa Marehemu wote na wale waliobaki majeruhi , akiomba neema ya upatanisho kati ya watu wa Ukraina na Poland.
Na mwisho alimwomba Mama Bikira Maria , daima azitazame kwa macho yake ya kimama familia za wale waliokuwa wakimsikiliza.









All the contents on this site are copyrighted ©.