2013-07-13 08:54:06

Akaunti zote za Monsinyo Nunzio Scarano zataifishwa!


Padre Federico Lombardi, Msemaji mkuu wa vatican anabainisha kwamba,, Mahakama ya Vatican imetaifisha akaunti zote zilizokuwa zinamilikiwa na Monsinyo Nunzio Scarano, ambaye hivi karibuni alivuliwa nyadhifa zake kutokana na tuhuma za kujihusisha na usafirishaji wa fedha chafu, kashfa ambayo inameihusisha pia Benki ya Vatican.

Fedha zote zilizohifadhiwa na Monsinyo Scarano kwenye Benki ya Vatican zimetaifishwa na kwamba, kuna uwezekano mkubwa kwa baadhi ya watu kuhusishwa na uchunguzi unaoendelea kwa kasi kubwa.

Wakati huo huo, Uongozi wa Benki ya Vatican umemteua meneja atakayekagua akaunti zilizoko Benki ya Vatican na wateja wake ili kujiridhisha kwamba, hakuna wajanja wachache wanaoweza kutumia Benki ya Vatican kwa ajili ya kutakatisha fedha haramu. Rais wa Benki ya Vatican Bwana Ernst Von Freuberg anasema hapa hakuna atakayevumiliwa!







All the contents on this site are copyrighted ©.