Papa Francisko ashiriki kikao cha kwanza cha Tume ye Benki ya Vatican
Kwa mara ya kwanza Tume ya Kipapa ya Benki ya Vatican imefanya kikao chake kwenye
Makazi ya Domus Sanctae Marthae yaliyoko mjini vatican na kuhudhuriwa na Baba Mtakatifu
Francisko. Kikao hiki kimehudhuriwa pia na viongozi waandamizi wa Benki ya Vatican,
IOR.
Katika mkutano huu, Baba Mtakatifu amewatia moyo wajumbe kuendelea na
kazi yao kwa umakini mkubwa kwa ajili ya mafao na ustawi wa Kanisa. Mkutano huu umefanyika
Jumatano, tarehe 10 Julai 2013.