Adhabu ya kifo, ni kinyume cha haki msingi za binadamu!
Jumuiya ya Mtakatifu Egidio yanye Makao yake Makuu mjini Roma, imekuwa mstari wa mbele
kuihamasisha Jumuiya ya Kimataifa kufuta adhabu ya kifo kwani adhabu hii ni kinyume
cha haki msingi za binadamu na badala yake kuangalia uwezekano wa kutoa adhabu mbadala.
Hadi sasa
kuna mafanikio makubwa yaliyokwisha kupatikana kutokana na harakati hizi, lakini bado
Jamii inapaswa kufundishwa ili kutambua kwamba, haki, amani, msamaha na upendo ni
fadhila fungamanishi. Adhabu ya kifo haimtendei haki mtuhumiwa. Ni maneno ya MS Queen
Said, Mratibu wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio nchini Tanzania katika mahojiano maalum
na Radio Vatican. Anasema, Jamii inapaswa kutambua athari za adhabu ya kifo, ili kusimama
kidete kulinda na kutetea uhai ambayo ni zawadi kubwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu.