2013-07-10 09:06:47

"Nimeguswa na Ibada ya Misa Takatifu na Baraka kutoka kwa Papa Francisko, zawadi kubwa katika hija ya maisha yangu ya imani"


Francis Kilenga, Afisa Miradi wa Shirika la Wamissionari wa Damu Azizi ya Yesu, Vikarieti ya Tanzania, yenye makao yake makuu mjini Dodoma katika mahojiano na Radio Vatican anakiri kwamba, kati ya matukio makubwa yaliyogusa hija ya maisha yake ni kushiriki Ibada ya Misa Takatifu pamoja na kupata baraka za Baba Mtakatifu Francisko, Jumapili tarehe 7 Julai 2013. RealAudioMP3

Francis Kilenga anasema kwamba, hili ni tukio ambalo kwa hakika atalikumbuka katika hija ya maisha yake ya kiroho na kwamba, limeacha chapa ya kudumu katika maisha yake kama Mkristo, hasa wakati huu Mama Kanisa anapoadhimisha Mwaka wa Imani.

Mzee Kilenga alikuwa nchini Ujerumani na Italia kama sehemu ya shughuli zake kwa ajili ya kujadiliana na Mashirika mbali mbali ya Misaada ya Kanisa Katoliki kwa ajili ya kuongezea nguvu katika mchakato wa utoaji wa huduma makini, wakati huu Shirika la Wamissionari wa Damu Azizi ya Yesu, linapojielekeza kusikiliza kilio cha damu, kutoka kwa maskini na wote wanaosukumizwa pembezoni mwa Jamii.







All the contents on this site are copyrighted ©.