2013-07-10 11:19:04

Miaka miwili ya Uhuru wa Sudan ya Kusini: Adhabu ya Kifo ifutwe!


Katika Maadhimisho ya Kumbu kumbu ya Mwaka wa Pili, Tangu Sudan ya Kusini ilipojitwalia uhuru wake, hapo tarehe 9 Julai 2011, wadau mbali mbali nchini humo, wanaitaka Serikali kufutilia mbali adhabu ya kifo. Ombi hili limetolewa na Wanashirika wa Comboni wanaofanya utume wao nchini Sudan ya Kusini, baada ya watu kadhaa kuhukumiwa na hatimaye kunyongwa baada ya kupatikana na kosa la mauaji kunako mwaka 2012.

Wamissionari hao wanaitaka Serikali kulivalia njuga tatizo la wizi wa mifugo ambalo kwa sasa linawanyima watu wengi usingizi. Katika Maadhimisho ya Miaka miwili ya Uhuru wa Sudan ya Kusini, Waamini wa Kanisa Katoliki nchini Sudan walifunga na kusali kwa ajili ya kuombea, toba, haki, amani, upendo na upatanisho wa kweli nchini Sudan ya Kusini baada ya vita na kinzani zilizosababisha utengano na madonda makubwa ya chuki na uhasama miongoni mwa wananchi wa Sudan.







All the contents on this site are copyrighted ©.